Kampuni
ya GM (General Motors) ya nchini Marekani imetangaza aina za magari
ambayo yanatarajiwa kutoka mwaka 2015 ambayo yatakuwa yameunganishwa na
huduma ya 4G LTE na kumuwezesha mtumiaji wa gari kuweza kutumia huduma
za internet popote atakapo kuwepo.
Hata hivyo, huduma hiyo ya 4G LTE itakuwa ikitolewa na
kampuni ya AT&T LTE na gari aina ya Buick ndiyo gari la kwanza
ambalo litatoka likiwa na limeunganishwa na huduma hiyo.
Mtumiaji ataweza kunuanua kifurushi cha kuanzia 200MB kwa mwezi kwa $5 na pia 5GB kwa mwezi kwa $50.