Nchi ya China ambayo hivi karibuni imekua tishio katika
masuala ya kiteknolojia imeongoza duniani kwa kuwa na Kompyuta zenye
uwezo mkubwa zaidi (Super Computers) aina ya Tianhe-2 zenye uwezo wa
kufanya mahesabu makubwa sana kwa sekunde (Quadrillions of calculations
per second).
Kompyuta izo za aina ya Tianhe-2 zilitengenezwa na chuo
kikuu uko china kijulikanacho kama National University of Defense
kushirikiana na na kampuni ya China ya masuala ya IT ijulikanayo kwa
jina la Inspur.
Hata hivyo, China imeongoza kwa kuwa na kompyuta zenye
uwezo mkubwa zaidi duniani lakini Marekani ndo inaongoza kwa kutengeneza
kompyuta nyingi zaidi za uwezo mkubwa.