Wakati Tanzania kukiwa na kampeni ya kukomesha tabia za kusambaza ujumbe mbaya kwa simu ya mkononi au mtandaoni tuliyoipa jina la ‘Delete Futa Kabisa’, serikali ya Jamhuri ya Afrika Magharibi imeamua kupiga marufuku kabisa kutumiana ujumbe wowote.
Uamuzi huo umekuja kutokana na sababu zilizotajwa kama ni kuhakikisha
ulinzi na usalama baada ya kupitia katika kipindi cha zaidi ya mwaka
mmoja wakiwa katika vita ya kidini.
Serikali ya nchi hiyo imetoa tamko rasmi baada ya waandamanaji
kufurika katika mitaa ya mji mkuu, Bangui huku wakihamasishana kupitia
jumbe za simu za mkononi kufanya maandamano makubwa zaidi.
Waandamanaji hao wanataka serikali ya mpito ya nchi hiyo iliyoingia madarakani January mwaka huu kujihuzuru.
Vita ya kidini nchini humo ilianza mwaka jana baadaya Michel Djotodia
aliyekuwa raisi wanchi hiyo ambaye ni muumini wa dini ya kiislamu
kujihuzuru na kukabidhi madaraka kwa watu wengi nchini humo ambao ni
waumini wa imani ya kikristo.