KOREA YA KASKAZINI YALIPUA MABOMU MAWILI YA NYUKLIA LEO ASUBUHI

Korea ya Kaskazini imelipua mabomu mawili ya nyuklia kwenye bahari ya Mashariki (bahari ya Japani) asubuhi ya leo kwa malengo ya kile ambacho Mail Online inahisi ni kuonesha mbwembwe kwa raisi wa China, Xi Jimping aliyetembelea Korea ya Kusini ambayo ni adui mkubwa na Korea ya kaskazini.
Wizara ya ulinzi ya Korea ya Kaskazini imeiambia AFP kuwa mabomu hayo yamelipuliwa kuelekea baharini na si kwingineko. Inaongeza kwa kusema,
"Mabomu yote yalitua baharini ingawa kiukweli yalivuka mipaka" .
Hata hivyo, wizara hiyo haikusema aina ya mabomu hayo yaliyolipuliwa. Lakini Yonhap News Agency inadai kuwa yalikuwa ni mabomu ya nyuklia lakini yenye uwezo mdogo sana kwani yanafika umbali upatao kilimita 500 ambazo ni sawa na maili 300 peke yake.
Hata hivyo, waziri wa ulinzi wa Japani, Itsunori Onodera amewaambia wanandishi wa habari kuwa Korea ya Kaskazini imerusha mabomu mengi sana na siyo mawili kama inavyodai. Ameongezea kuwa serekali ya japani imepinga vikali kitendo hicho kwa kupitia ubalozi wao uliopo Beijing nchini China.
Mail Online inadai kuwa achilia mbali suala la kuonesha mbwembwe kwa raisi wa China,  inaonesha dhairi kuwa vikosi vya Korea ya Kaskazini vilikuwa viliwalenga wanajeshi wanaoiwakilisha Marekani wakiwa katika mataifa ya Mashariki ya mbali.
Maafisa  na wanajeshi wa Jeshi la wananchi  wa Korea wakila kiapo cha kupambana na marekani kufa na kupona katika maadhimisho ya 64 ya kuanza kwa vita vya Korea .