Huu ni mfano wa sanduku la agano ambalo wana wa Israel waliambiwa watengeneze na Mussa wakiwa nyikani wakitoka Egypt (Misri) wakielekea promised land (Nchi ya ahadi). Sanduku hilo lilikuwa ni kama box la mbao lililotengenezwa na aina moja ya mbao inayoitwa (acacia wood)
iliyofunikwa na dhahabu. Lilikuwa la urefu wa 1.15 metres, upana wa 0.7
metres na kimo cha 0.7 metres. Ilikuwa inabebwa na mishikio miwili
mirefu ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa mbao hiyo ya acasia ambazo
pia zilikuwa zimefunikwa na dhahabu. Juu ya sanduku kuliwekwa makerubi
wawili waliokuwa wamegeukiana mabawa yao yakiwa yamegusana. Uwepo wa
Mungu haukuwepo ndani ya sanduku bali ulikuwa juu yake katikati ya hao
makerubi. Uwepo wa Mungu juu ya sanduku hilo ulikuwa kama nuru. Kuhani
mkuu alipaswa kufunika macho asiione nuru hiyo ("hakuna mwanadamu anionaye na akaishi"
Kutoka 33 : 20) kila alipokuwa akiingia lilipokuwa sanduku ambapo ni
patakatifu pa patakatifu. Hapa ndipo ambapo Mungu alipokuwa akiionana na
Musa. Sanduku hili lilikuwa likibebwa na wana wa Walawi pekeyake hakuna
mwingine aliyeruhusiwa kulishika, yeyote aliyedhubutu kulishika
pasiporuhusiwa alikufa papohapo. Hao makerubi wawili wanawakilisha
utukufu wa Mungu. Ndani ya sanduku hili kulikuwa na:
- Mawe mawili yaliyokuwa yameandikwa amri kumi za Mungu
- Fimbo ya Aron iliyoota mauwa
- Chombo cha dhahabu kilichokuwa na manna waliyokula wana wa Israel nyikani
Sanduku
hilo lilikuwa linakaa patakatifu pa patakatifu, chumba cha ndani kabisa
katika hema la kukutania. Aliyekuwa anaruhusiwa kuingia mahala hapo
lilipokuwa sanduku hilo ni kuhani mkuu na alikuwa anaruhusiwa kuingia
mara moja kwa mwaka. Kabla ya Kuhani mkuu kuingia patakatifu pa
patakatifu alikuwa ni lazima aingie na damu ya mwana kondoo kwa niaba ya
dhambi zake yeye mwenyewe na dhambi za wana wa Israel.
Sanduku la agano lilikuwa ndani ya hekalu lililojengwa na Solomon mpaka hekalu hilo lilipokujwa kuvunjwa mikononi mwa utawala wa Babylon ukioongozwa na Nebuchadnezzar. Kilichotokea kwa sanduku hilo hakijulikani ingawa haiwezekani kuwa lilichukuliwa na majeshi ya Babylon
kama vilivyochukuliwa vyombo vingine vya hekalu kwasababu katika list
ya vitu walivyovichukua sanduku la agano halikutajwa. Kulingana na
baadhi ya vyanzo vya habari inasemekana kuwa mfalme Josiah, mmojawapo wa wafalme wa mwisho kutawala enzi za hekalu la kwanza, kutokana na unabii uliokuwa umetolewa alijua kuwa Jerusalem itavamiwa na Babylon,
akalificha sanduku la agano. Alipolificha sanduku imekuwa kitendawili.
Chanzo kingine cha habari kinasema kuwa mfalme Solomon alionyeshwa kuwa
Hekalu litakujwa kuvunjwa na majeshi ya Babylon, kwahiyo akaandaa pango
karibu na bahari ya shamu (dead sea) ambapo Josiah akaja kulificha sanduku. Na pia inasemekana nabii Yeremia (Jeremiah)
alilificha sanduku chini ya Hekalu lililojengwa na Solomon. Na hata
kuna tetesi ya kuwa hapa Tanzania kwenye misitu ya monduli kuna chombo
chenye mfano wa sanduku la agano, ambacho kiliachwa hapo na majeshi ya
Ujerumani enzi za ukoloni. Inasemekana kuwa chombo hicho kina miujiza na
mambo mengi ya ajabu na kutisha.
Je wewe
mdau unasemaje kuhusu chombo hiki cha jabu? Kwa mtazamo wako unadhani
kipo wapi? Toa mchango wako kuhusu chombo hiki cha ajabu na kihistoria.