Kampuni ya Soft Bank ya nchini Japan imetengeneza Robot ambayo ina uwezo ya kuwasiliana na kusoma hisia za mwanadamu.
Robot hiyo
iliyopewa jina la Pepper inadaiwa kuwa ina uwezo wa kufikiri kama
mwanadamu na kufanya kile mtu atakachomwambia na uwezo wa kufanya
shughuli mbalimbali kama binadamu.
Pepper
mwenye urefu wa futi nne ni Robot ya kwanza yenye moyo ambapo ina uwezo
kutambua sauti, ishara, maneno kupitia programu ya akili bandia
iliyofungwa au ‘emotional engine’.