MUIMBAJI WA CHAMBER SQUAD MEZ-B AFARIKI DUNIA==>SOMA ZAIDI

Muimbaji wa kundi la Chamber Squad, Maze B, amefariki leo saa nne asubuhi, kwa mujibu wa mtu aliyekuwa akimuuguza.
 
Msanii huyo aliyewahi kufanya vyema na wimbo wake ‘Fikiria’ alikuwa amelazwa katika  hospitali ya Mwananchi mjini Dodoma.

Mez B aliyezaliwa kwa jina la Moses Bushagama alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Pneumonia.
 
Hivi karibuni aliongea na E-News ya EATV na alikuwa anaendelea vyema:
 
“Nilikuwa na tatizo la Pneumonia tokea mwezi wa 12 nikawa nipo vizuri nilivyo kuja tena Dodoma hali ikabadilika ndo nipo hospitali nimelazwa nasumbuliwa na maumivu ya kichwa na shingo,” alisema.
 
“Nategemea kuruhusiwa muda wowote na sasa hivi naendelea vizuri.”
 
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Wabunge Wataka Wanafunzi Wafunzwe Somo La Ngono==>SOMA ZAIDI

Shule zote za serikali zikiwemo za msingi na zile za upili nchini Uingereza zitalazimika kufunza somo la ngono na uhusiano SRE ,wabunge wa taifa hilo wamesema katika ripoti yao.
Kamati ya elimu katika bunge la Uingereza ilianzisha uchunguzi baada ya kubainika kuwa zaidi ya thuluthi moja ya shule zilikuwa zikishindwa kutoa mafunzo ya somo hilo kwa aumri unaohitajika.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Graham Sturat amesema kuwa vijana wadogo wana haki ya kupata habari ambazo zitahakikisha usalama wao.
Serikali imesema kuwa itaangazia matokeo ya ripoti hiyo.
Mwaka 2013 ripoti ya bunge hilo ilisema kuwa masomo ya kibinafsi,ya kijamii ,afya na elimu ya kiuchumi ambapo somo hilo la ngono limehusishwa yanahitaji kuimarika katika asilimia 40 ya shule.
Wabunge hao wamesema:Hali hii haitakubalika katika masomo mengine licha ya kuwa harakati za serikali kuimarisha masomo hayo ni za kiwango cha chini.
Je,unakubaliana na wazo la bunge la Uingereza kuwafunza watoto wa shule za msingi somo la ngono na uhusiano? Kwa maini yako basi ingia katika mtandao wetu wa faceboo katika bbcswahili.
 >>BBC

Chupi Inayobana Yamtoa M'bunge Bungeni...SOMA HAPA

Mbunge mmoja wa Canada alitoa sababu ambayo haijawahi kusikika iliomlazimu kutoka bungeni kwa haraka.
Amesema kuwa suruali yake ya ndani ndio iliomlazimu kuondoka mapema kwa kuwa ilikuwa ikim'bana.
Mbunge huyo wa upinzani Pat Martin alimwambia Spika kwamba vazi hilo lilimbana sana na kumzuia kuweza kuendelea na kikao cha kupiga kura.
Hatahivyo alifanikiwa kurudi kwa wakati na kupiga kura yake.
Baadaye mtandao wa twitter ulijaa ujumbe wa kisa hicho.
Mbunge huyo alizua ucheshi miongoni mwa wabunge wenzake liposema kwamba alinunua suruali hiyo kwa bei ya chini bila kujua kwamba ilikuwa ndogo.
Spika wa bunge hilo alisema kwamba alimuagiza mbunge huyo kuketi chini wakati alipotaka kutoka.

Sina mtoto wala watoto, Sijawahi toa Kizazi ili Nifanikiwe Kifedha ,Lady Jaydee

Lady Jaydee ameendelea kujibu maswali ya mashabiki wake kupitia Instagram, na maswali mengine aliyokutana nayo ni kuhusu kama ana mtoto au ameasili mtoto ambaye huonekana kwenye kipindi chake cha ‘Diary Ya LadyJaydee’ kinachorushwa kupitia EATV.

SWALI: Una watoto wangapi?
JIBU : Sina mtoto wala watoto

SWALI: Utazaa lini?
JIBU : Sijajua mpk sasa nitazaa lini, ila siku yoyote ile ikitokea naweza kuzaa

SWALI: Kwanini huna mtoto /watoto?
JIBU : Sina mtoto /watoto sababu sijawapata, nikipata nitakuwa nao.

SWALI: Tunaskia ume adopt mtoto ? Na mtoto tunaekuona nae ni wa nani?
JIBU : Sija adopt mtoto, mtoto mnae muona ana shine like a star, ananiita Shangazi, ninaishi nae sbb ya ukaribu wa shule anayosoma ,Tunaishi wawili tu, mimi na yeye
Anaitwa “Mokonyo Yvonne Mbibo” Ni binti wa mdogo wangu @dabomtanzania

SWALI: Tunaskia una mtoto mkubwa ulimzaa ukamuacha kijijini Shinyanga /Musoma
JIBU : Sina mtoto niliemuacha kijijini, sijawahi kuishi kijijini.
Sijawahi kuishi Musoma, kwetu ni Bunda na huwa naenda ikitokea misiba kuzika, sijawahi kuishi huko zaidi hata ya miezi 2 Shinyanga niliozaliwa ni mjini

Nilihama Shinyanga, kuja Dar es salaam nikiwa na miaka 11
Sijawahi kurudi kuishi huko tena zaidi ya kwenda kusalimia.

SWALI: Tunaskia huzai, ulitoa kizazi ili ufanikiwe kifedha?
JIBU : Sijatoa kizazi na sifanyi kitu chochote unusual ili kupata mafanikio

Angalizo : Mwenyezi Mungu hadhihakiwi, so stop calling me names. …….Kesho anaijua yeye, lolote pia linaweza kutokea. Accept me the way I am”

STYLE YA MKAO WA BEUTFULL ONE ALIVYOJIBINUA WAZUA GUMZO MTANDAONI...ONA HAPA==>

Nimepitia ukurasa wa Malkia wa Insta nikakutana na Picha hiyo ya Wema Akiwa ameegemea gari aliyopewa kama zawadi na Martin Kadinda siku ya Birthday yake huku akiwa amekibinua cha chini ya mgogo ..

Baadhi ya watu wamemsifia na wengine kujaribu kumshauri.Soma Comments hapo chini kutoka ukurasa huo:

dicksonmgesy
Jaman tumpe chachu ya maendeleo sio kumsifia zari hana tako ila ana mali na hela mpaka anatamani kujiteka. Huku sifa kuwa na tako lisilo na kitu. Hayaaaaa

__dat__gal__
Sure @dicksonmgesy alf hcho kigali xx cha uyo wemaa maskin kawaidaaaa xnaaaa yani wema hana radhaaa hanaaa

dicksonmgesy
 tangu awe mis mpaka leo ana nini? Angalia wenzake kama jokate hana jna kubwa ila ana mafanikio yeye anaishi maisha ya kuigiza yuko wap? Afike mahali ajitambue aache kufanya maonyesho sifa sio maendeleo tangu tuanze kumsifia tumeshawahi kumpa hata mia?

Samgal
aache maisha ya maigizo, tunataka kuona maendeleo sio skendoz

theysay0
@dicksonmgesy kila mtu na baraka zake na kwa wakati wake. How many people they hv bn trying and trying and reach their goals. Her time will come.

hashypapito
Nilisikia wakisema wema shapeless kumbe walimaanisha shapeclass daaaah nampendaga bureeee

wildsweetcandies
Haters don't really hate you @wemasepetu , they hate themselves; because you're a reflection of what they wish to be.

Kingwendu 2015 kuingia bungeni kuwakilisha wananchi wake ..SOMA HAPA

Mwigizaji mkongwe wa vichekesho hapa Bongo, Rashid Mwinshehe "Kingwendu", amesema anajiandaa Kugombea Ubunge 2015 Kupitia Chama ambacho amedai Kuwa anaona Kinapendwa na Watanzania wengi bila ya Kutaja Jina la Chama hicho wala Jimbo atakalogombea.
 
Wataalamu wa Masuala ya Kisiasa Nchini, wameitafsiri Kauli hiyo ya Kingwendu Kwa Mitazamo tofauti, huku Wengi Kati yao Wakisema Kuwa Upinzani Una Nguvu Kubwa hivi sasa hapa Nchini, hivyo Sio ajabu Kwamba yawezekana Msanii huyu amevutiwa na Kuamua Kujiunga na Chama fulani Cha Upinzani Ili aendeshe harakati za Ukombozi wa Taifa hili.
 
Akizungumza na Mwandishi wa Tanzania Daima, Kingwendu alisema, "Ninajiandaa Kugombea Ubunge 2015 Kupitia Chama ninachoona Kinapendwa na Watanzania wengi Kwenye Jimbo ambalo ntalitaja hapo baadae Wakati Utakapofika...

"Bado ninafanya Mazungumzo na Washauri wangu wa Karibu Kuhusiana na Swala, nadhani ntaliweka Wazi muda Ukifika..."
 
Source:Tanzania Daima

Wezi wa kompyuta wameiba dola bilioni 1....SOMA HAPA

Genge la wezi wa kompyuta limefanikiwa kuiba takriban dola bilioni moja kutoka kwenye akaunti za wateja wa mabenki 100 katika mataifa 30.

Kampuni inayosimamia usalama wa programu ya kompyuta inayohakikisha data ya wateja iko salama Kaspersky Lab imesema katika ripoti yake maalum.

Ripoti hiyo inaelezea mbinu mpya ya wezi wa Kompyuta wanaotumia mbinu mpya ya kudakua nambari za akaunti za wateja za siri kabla ya kuingia na kupora pesa .

Kaspersky imesema kuwa wizi huo ulianza mwaka wa 2013 na bado unaendelea hata leo kwani mabenki yote yalioathirika hayana uwezo wa kuwazuia wezi hao .

Hadi kufikia sasa ripoti hiyo inadai kuwa takriban dola bilioni moja zimeporwa kutoka kwenye akaunti za wateza.

Genge hilo la wezi, lililoanzia shughuili yake nchini Urusi, Ukraine na pia Uchina ndilo linalolaumiwa kwa wizi huo.

Kampuni hiyo ya Kaspersky inasema inafanya juhudi za kuzima wizi huo kwa ushirikiano na polisi wa kimataifa Interpol na polisi wa bara ulya Europol .

Kwa mujibu wa ripoti hiyo mabenki katika mataifa 30 yakiwemo, Russia, Marekani , Ujerumani , Uchina, Ukraine na Canada yameathirika pakubwa.
Kamanda wa kikosi cha polisi wa kimataifa Interpol bwana Sanjay Virmani, amesema kuwa wezi wataendelea kutumia upungufu wa miundo msingi katika sekta ya uchumi wa mataifa husika hadi pale kutaibuka umoja wa kuzuia mapengo.

Kaspersky hata hivyo inasema kuwa genge hilo linalenga mabenki bila ya kuwaibia watu binafsi.

genge hilo kwa jina Carbanak, linatumia mbinu ya kuambukiza virusi kwenye mashine za benki ikiwemo kamera za CCTV ilikunakili kila kitu kinachoandakiwa kwenye kompyuta.

Kutokana na uweledi wao genge hilo lilituma pesa kwenye account zao huku wengine wakiamrisha mmitambo ya kutoa pesa ATM kumimina pesa bila kikomo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kila tukio la wizi lilihusisha takriban dola milioni kumi.

MTAALAM WA SILAHA ZA KEMIKALI AUWAWA==>SOMA HAPA

 Jeshi la Marekani linasema kuwa mtaalamu mmoja wa silaha za kemilkali aliyekuwa akifanya kazi na kundi la Islamic State ameuawa kwenye mashambulizi ya muungano nchini Iraq.
Marekani inasema kuwa kifo cha mwanamume huyo kwa jina Abu Malik kitavuruga uwezo wa kundi hilo wa kuunda na kutumia silaha za kemikali.
Abu Malik anaripotiwa kufanya kazi kama mtaalamu wa silaha za kemikali kwa rais wa zamani wa Iraq Sadam Hussein kabla ya uvamizi ulioongozwa na Marekani mwaka 2003.
Kundi la Islamic State hudhibiti maeneo makubwa nchini Syria ambapo serikali imekuwa ikiharibu silaha za kemikali.

Daktari afungwa kwa ukeketaji Misri..==>soma hapa

Katika kesi cha kipekee nchini Misri, daktari mmoja ametiwa mbaroni kwa kosa la kumkeketa msichana mwenye umri wa miaka kumi na tatu.
Wakereketwa wanaopinga tabia ya kuwakeketa watoto wa kike, walishtuka baada ya mahakama kumwachilia huru Daktari Raslan Fadl mwezi Novemba mwaka jana.
Lakini baada ya kesi kusikizwa upya, amehukumiwa zaidi ya miaka miwili gerezani.
Ingawa ukeketaji wa wasichana ulipigwa marufuku miaka sita iliyopita nchini Misri, zoezi hilo bado linaenea pakubwa.
Wale ambao wanajaribu kupambana na ukatili huo wameelezea hukumu ya Daktari Fadl kuwa ni ushindi mkubwa kwao.

ALIYEDONDOSHA BOMU LA NYUKILIA HIROSHIMA-JAPAN AFARIKI DUNIA


Kapteni Theodore Van Kirk, katikati, na wenzake wakati wakirejea kutoka katika misheni ya Hiroshima, Japan Agosti 6, 1945. Kushoto kwake ni Kanali Paul Tibbetts kamanda wa msafara.

MWANAANGA wa mwisho katika  ndege aina ya B-29  (Enola Gay) iliyopiga mji wa Hiroshima uliopo Japan  na bomu la nyukilia (“Little Boy”) mji wa Hiroshima, amefariki dunia.Kwa mujibu wa The Atlanta Journal-Constitution,Mwanaanga huyo Theodore “Dutch” Van Kirk, 93, alikuwa navigeta  wa ndege hiyo ambayo Agosti 6 1945 ilidondosha bomu hilo na kumaliza vita vya dunia.

Baada ya kifo cha   Morris Jeppson, mwaka 2010,Van Kirk alikuwa ndiye mpiganaji pekee aliyebaki kati ya wapiganaji dazeni walishiriki katika misheni hiyo.

Kwa miaka mingi alikuwa akiishi katika makazi ya wastaafu  huko Stone Mountain na walikuwa akiishi na James Starnes,  navigeta wa USS Missouri ambaye alipokea ujumbe wa kujisalimisha rasmi kwa Japan, Septemba 2, 1945.

Starnes, amesema rafiki yake alikufa Jumatatu baada ya kuwa hospitalini kwa wiki kadhaa.

Alisema kwamba kwa mara ya kwanza kwa miaka mingi alidondosha chozi kwa rafiki yake huyo ambaye kwa pamoja kwa nyakati tofauti walikuwepo wakati wa kuandika historia ya dunia.