Imeripotiwa kuwa chui mwenye hasira na njaa aliingia majini
na kupanda boti ya mvuvi aliyetajwa kwa jina la Shushil Manjhi huko
Kolkata, India na kuondoka nae.Taarifa
zilizoripotiwa na vituo vya nchini India vinaeleza kuwa, mvuvi huyo
alikuwa na watototo wake wawili (wa kike na wakiume) wakijaribu kutafuta
kitoweo karibu na hifadhi ya taifa ya Sunderbans yenye wanyama
wakali.Mwanae wa kiume, Jyotish alieleza kwa njia ya simu kuwa chui huyo
alirukia boti na kumkamata baba yake shingoni kwa upande wa nyuma na
kuanza kumburuza akiondoka nae akielekea msituni.“Alimrukia baba yangu
kwa haraka mgogoni na kung’ata kwa nguvu kabla hajatokomea nae msituni.”
Alieleza.Mtoto huyo anaeleza kuwa baada ya chui huyo kumkamata baba
yake, yeye na mdogo wake walijaribu kumpiga na fimbo na visu walivyokuwa
navyo lakini hakuweza kumuachia.Tukio hilo linatoa picha ya maisha duni
ya wananchi masikini wa eneo hilo ambao licha ya kuwa na hatari kubwa
ya kuuawa na wanyama wakali, hali ngumu ya maisha huwasukuma kuingia
msituni kusaka kitoweo au chochote licha ya kwamba ni kinyume cha sheria
kufanya uvuvi katika eneo la hifadhi ya wanyama.Inaelezwa kuwa samaki
wanaopatikana katika hifadhi hiyo hunuliwa kwa pesa nyingi katika miji
ya jirani na vijiviji vya eneo hilo.
Chui apanda boti na kumshambulia mvuvi akiwa na watoto wake.
Unknown
KIMATAIFA